Kulingana na Mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Mkutano wa Wakurugenzi na wasimamizi wa Seminari ya Qom na Ayatollah Alireza Arafi, Mkurugenzi wa Seminari zote nchini (Iran), ulifanyika usiku wa Jumatatu, Machi 3, katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Dar al-Shafa....
Ayatollah Arafi wakati wa hotuba yake katika mkutano huu akirejea Aya ya 186 ya Surah al-Baqarah
«وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّی قَرِیبٌ ۖ أُجِیبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْیَسْتَجِیبُوا لِي وَلْیُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ یَرْشُدُونَ»
Alisema: Aya hii ni miongoni mwa Aya chache za Qur’an kuhusu Dua (Maombi), na ina mambo muhimu sana. Akasema: Kwa upande mmoja, Aya hii inaonyesha uhusiano kati ya Mja na Mola wake, na kwa upande mwingine, inaeleza kuhusu uhusiano kati ya Muombaji na Muombwaji kuwa ni uhusiano maalum.
Akisema (kufafanua) kuwa uhusiano kati ya mManadamu na Mwenyezi Mungu uko karibu sana kwa mtazamo mmoja, na uko mbali sana kwa mtazamo mwingine, alisema: Uhusiano huu uko mbali sana kwa mtazamo mmoja, kwa sababu kuna daraja nyingi, na kutokana na mtazamo mwingine, kwa sababu ya bahthi (au utafiti wa kielimu kuhusu) sababu (العلة) na kilichopo nyuma ya sababu (ما وراء العلة) na udhihirisho (التجلي), na kwamba uwepo wote wa Ulimwengu na Mwanadamu umejaa udhihirisho wa ki-Mungu, kwa upande huu uhusiano kati ya Mwanadamu na Mwenyezi Mungu uko karibu sana. Kwa upande mmoja, udhihirisho wa Mwenyezi Mungu hupenya na kuwepo katika kina cha uwepo wa Wanadamu, na kwa upande mwingine, udhihirisho huo uko mbali sana kiasi kwamba haiwezekani hata kuelezewa. Huu ni uhusiano wa Mja na Mola wake au uhusiano wa kila kiumbe na Muumba wa kweli.
Mkurugenzi wa Seminari nchini, aliashiria juu ya aina nyingine ya uhusiano kati ya Mwanadamu na Mwenyezi Mungu unaoitwa uhusiano wa kisheria na kusema: Katika aina hii ya uhusiano, kiumbe ni mtumishi (mja) mwenye akili, ni mwenye ufahamu na chaguo (hiari), ambaye amewekwa katika nafasi ya mazungumzo na Mwenyezi Mungu. Huu sio uhusiano kati ya Muumba na Kiumbe, bali ni uhusiano kati ya Mwombaji na Muombwaji, na huu ni mzunguko maalum na uhusiano maalum ambao umeanzishwa (baina ya Muombaji na Muombwaji), na Mja mimi nimepata taufiki hii ya kuwa katika uwanja huu wa dua.
Katika sehemu ya pili ya hotuba yake, Mkurugenzi wa Seminari aliwaambia Wasimamizi (Mameneja) wa Seminari ya Qom: Seminari, hasa Seminari ya Qom, ni dhamana ya kihistoria yenye thamani ambayo tumeichukua, na mabega yetu hayawezi kubeba mzigo wa uaminifu huu (amana hii) kwa urahisi.
Alisema kwamba kuna hadithi nyingi kuhusu utakatifu, thamani na heshima ya ardhi ya Qom hata kabla ya Uislamu na akasema: Katika historia ya miaka 1240 ya Qom, tangu zama za Imamu Sadiq (a.s) wakati uhamaji ulipoanza na familia ya Ash’ari na familia nyingine nyingi kutoka Rawats na Muhaddithin kufika Qom, Mji huu ulipata sharafu na heshima maradufu, na kwa maziko ya Hadhrat Fatima Masoumah (s.a) Mji huu uliongezewa zaidi heshima hii.
Maoni yako